Wanajeshi wa India na Pakistan wakabiliana mpakani

A picture of a Chinese and Indian soldier. Haki miliki ya picha AFP
Image caption Shirika la habari la PTI lilisema kwa wanajeshi walirusha mawe na kusababisha majeraha madogo pande zote,

Makabiliano yametokea kati ya wanajeshi wa India na Pakistan sehemu ya mpaka inayozozaniwa magharibi mwa Himalaya.

Shirika la habari la PTI lilisema kwa wanajeshi walirusha mawe na kusababisha majeraha madogo pande zote, wakati wanajeshi wa China walijaribu kuingia himaya ya India karibu na ziwa Pangong.

China inasema kuwa wanajeshi wake walikuwa ndani ya ardhi yake.

Nchi hizo mbili pia zinazozana katika eneo la Doklan ambalo linapakana na India, China na Bhutan.

PTI ilinukuu maafisa wa kijeshi wakisema kuwa makabiliano ya hivi punde , wanajeshi walipanga mlolongo kuwazuia wanajehsi wa China kuingia sehemu zinazodaiwa na India.

Afisa mmoja nchini India aliambia BBC kuwa hawezi kukiri wala kukataa ripoti hizo akisema kuwa visa kama hivyo hutokea.

Wizara ya mashauri ya nchi za kigeni wa China ilisema kuwa India ni lazima iondoe wanajeshi wake kutoka ardhi yake, ikisisitiza kuwa wanajeshi wake walikuwa ndani ya china wakati makabiliano hayo yalitokea.

Mada zinazohusiana