Watu 600 waokolewa, pwani ya Hispania

Wahamiaji wakijaribu kuingia Ulaya Haki miliki ya picha EPA
Image caption Wahamiaji wakijaribu kuingia Ulaya

Walinzi wa pwani ya Hispania wamewaokoa karibu watu mia sita kutoka katika vyombo mbalimbali vya usafiri majini ikiwemo, bota majahazi yaliyokuwa yakisafiri kutoka nchini Morocco.

Umoja wa Mataifa umesema zaidi ya watu elfu nane wamewasili nchini Hispania toka kuanza kwa mwaka huu.

Zaidi ya watu laki moja na 20 wanakisiwa kuzama maji wakijaribu kuelekea Ulaya.

Idadi kubwa ya watu inayokaribia laki moja walifanya safari za hatari kutoka Libya kwenda Italia tangu kuanza kwa mwaka huu.