Wafungwa 35 wauawa Gerezani, Venezuela

Eneo ambalo wafungwa hao wameuawa Haki miliki ya picha Atlas
Image caption Eneo ambalo wafungwa hao wameuawa

Gavana wa jimbo la Amazonas nchini Venezuela amesema zaidi ya wafungwa 35 wameuawa katika kile kilichoitwa ''Mauaji'' ndani ya gereza.

Kikosi maalumu cha jeshi cha wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi hiyo kimepelekwa kudhibiti hali ndani ya gereza katika mji mkuu wa jimbo hilo, Puerto Ayacucho.

Watu walioshuhudia tukio hilo wamesema walisikia milio ya risasi kwa saa kadhaa.

Hakuna kauli yoyote iliyotolewa na serikali mpaka sasa.