Mbunge wa kwanza Mwanamke Sudan, azikwa

Rais wa Sudan Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Rais wa Sudan

Maefu ya watu wamehudhuria mazishi ya mwanamke wa kwanza kuwa mbunge nchini Sudan.

Fatima Ahmed Ibrahim, mkominist, miaka yote ya umri wake amepigania haki za wanawake, hivyo kushinda tuzo mbalimbali za kimataifa.

Msiba wake umefanyika katika mji wa Omdurman, ambapo waombolezaji walimlazimisha waziri mkuu Bakri Hassan Salah na gavana wa jimbo la Khartoum Abdelrahim Mohamed Hussein, kuondoka katika msiba huo.

Ambapo walishiriki katika kupindua serikali mnamo mwaka 1989 ambapo Fatima Ahmed Ibrahim na wenzake walikimbia nchi.