Bi Mugabe aomba kinga ya kidiplomasia dhidi ya kesi

Mugabe na mkewe
Image caption Mugabe na mkewe

Serikali ya Zimbabwe imemuombea mkewe Mugabe kinga ya kidiplomasia dhidi ya kesi ya ushambuliaji inayomkabili nchini Afrika kusini , maafisa wa polisi wa taifa hilo wamesema.

''Grace Mugabe alikuwa bado yupo Afrika Kusini'' iliongezea wakipinga ripoti za awali kwamba alikuwa amerudi nchini Zimbabwe.

Mwanamitindo mwenye umri wa miaka 20 amemtuhumu bi Mugabe kwa kumshambulia katika hoteli moja mjini Johannesburg.

Polisi walitarajia kwamba bi Mugabe angejiwasilisha kwao mwenyewe siku ya Jumanne lakini hakufanya hivyo.

''Serikali ya Zimbabwe imewasilisha ombi la kumlinda kidiplomasia'', wizara hiyo ilisema katika taarafa yake.

Hatahivyo Afrika Kusini bado ilikuwa inataka kuhakikisha kuwa kinga hiyo amepatiwa kulingana na sheri, wizara hiyo iliongezea.

Mazungumzo yalikuwa yanaendelea na mawawikili wa Bi Mugabe na ubalozi wa Zimbabwe kuhusu swala hilo, ilisema taarifa.

Akizungumza mbele ya kamati ya bunge mapema, kaimu mkuu wa polisi Lesetja Mothiba alisema kuwa bi Mugabe ni shari aende mahakamni.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mwanamitindo aliyepigwa na bi Mugabe

Hajatoa tamko lolote tangu maafisa wa polisi waanze kumchunguza kuhusu madai hayo ya unyanyasaji.

Serikali ya Afrika Kusini inakabiliwa na shutuma kali iwapo itamwachilia huru bi Mugabe.

Hilo lilitokea 2015 wakati iliposhindwa kumkamata na baadaye kumkabishi rais wa Sudan Omar el Bashir katika mahakama ya ICC.