Wasichana Kenya waunda app kusaidia kukabili ukeketaji

Wasichana Kenya waunda app kusaidia kukabili ukeketaji

Kundi la wasichana mjini Kisumu, magharibi mwa Kenya wameungana na kuunda programu tumishi, yaani app, kwa jina iCut ya kusaidia kukabiliana na ukeketaji.

Cynthia na Purity wanasema wasichana wengi bado hawana ufahamu kuhusu ukeketaji na madhara yake.

Wameteuliwa kushindania tuzo mjini San Francisco, California ambapo wakifanikiwa wanasema watatumia pesa hizo kuboresha app hiyo na kuwasaidia wasichana walioathiriwa na ukeketaji.