Dangote: Nikiinunua Arsenal nitamfuta Wenger

Dangote anaorodheshwa kuwa mtu tajiri zaidi Afrika Haki miliki ya picha AFP
Image caption Dangote anaorodheshwa kuwa mtu tajiri zaidi Afrika

Mfanyabiashara tajiri raia wa Nigeria Aliko Dangote, ambaye anaorodheshwa kuwa mtu tajiri zaidi Afrika, amesema kuwa atamfuta kazi meneja wa Arsenal, Arsene Wenger, ikiwa atafaulu kuinunua klabu hiyo ya Uingereza, kwa mujibu wa shirika la Bloomberg.

Wakati wa mahojiano na shirika hilo, Bwana Dangote alisema kuwa atajaribu kununua klabu hiyo, wakati ujenzi wa kiwanda chake cha kusafisha mafuta cha gharama ya dola bilioni 11 mjini Lagos utakamilika.

Bw. Dangote anasema amekuwa shabiki wa Arsenal tangu miaka 1980.

Wenger ni mmoja wa mameneja wa kandanda wanaosifika sana barani Ulaya na hivi majuzi, alisaini mkataba wa miaka miwili na kuendelea kuwa na klabu hiyo kwa zaidi ya miongo miwili.

Kuna maoni tofauti kutoka kwa wafuasi wake, wengine wakisema kuwa klabu hiyo inahitaji meneja mpya ili kiweze kurejea hadhi yake.

Mada zinazohusiana