Tetesi za soka Ulaya Alhamisi 17.08.2017

Danny Rose Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Danny Rose

Tottenham hawapo tayari kupokea dau lolote kutoka kwa Chelsea kwa ajili ya Danny Rose, 27, huku Chelsea wakiwa tayari kumlipa mshahara mara dufu beki huyo. (Evening Standard)

Manchester United hawana mpango tena wa kumfuatilia Danny Rose, 27, huku beki huyo akitaka kwenda Old Trafford. (Daily Star)

Mwenyekiti wa Tottenham Daniel Levy amesema kiungo Dele Alli, 21, hauzwi hata kwa pauni milioni 150, huku Barcelona na Manchester City wakimfuatilia. (Sun)

Tottenham wamezidiwa kete na Lyon katika kumsajili kiungo wa Celta Vigo Pape Cheikh Diop, 20. Spurs walipanda dau la pauni milioni 9. (Daily Mail)

Chelsea hawajakata tamaa ya kumsajili Alex Sandro, 26, kutoka Juventus, lakini matumaini yao yapo kwenye mchezaji huyo kuwasilisha mwenyewe maombi ya kuondoka. (Evening Standard)

Chelsea wamepanda dau la pauni milioni 73 kumtaka Alex Sandro, lakini Juventus wamekataa. (Calciomercato)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Alex Sandro

Meneja wa Chelsea Antonio Conte yuko tayari kutoa pauni milioni 25 pamoja na marupurupu zaidi ili kumsajili Danny Drinkwater, 27, lakini Leicester wanataka pauni milioni 40. (Daily Mail)

Barcelona wamewapa Liverpool pauni milioni 118 kutaka kumsajili Philippe Coutinho. (Goal.com)

Barcelona wanakaribia kukamilisha usajili wa Ousmane Dembele, 20, kutoka Borussia Dortmund. (Daily Express)

Manchester City wamepanda dau la pauni milioni 60 kumtaka Alexis Sanchez, 28, wa Arsenal. Real Madrid pia wanamtaka Sanchez. (Don Balon)

Arsenal wamekataa dau la pauni milioni 45 kutoka Manchester City kumtaka Alexis Sanchez. (El Mercurio)

Image caption Alexis Sanchez

Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger amemuambia Alex Oxlade-Chamberlain, 24, kuwa anataka abakie Emirates "kwa muda mrefu" huku Chelsea, Liverpool na Manchester United wakimtaka winga huyo. (Sun)

Arsene Wenger amesema Alexis Sanchez, na Alex Oxlade-Chamberail huenda wakauzwa msimu huu. (Daily Star)

Aston Villa wanataka kumsajili kiungo wa Arsenal Jack Wilshere, 25. (Daily Mail)

Southampton wanakaribia kukamilisha usajili wa beki wa Lazio Wesley Hoedt, 23 kwa pauni milioni 15.4. (Daily Mirror)

Manchester United wapo tayari kumpa Zlatan Ibrahimovic, 35, nafasi ya kuwa kocha kama sehemu ya mkataba mpya. (Independent)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Zlatan Ibrahimovic

Napoli wamekataa dau la pauni milioni 55 kutoka kwa Barcelona la kumtaka mshambuliaji Lorenzo Insigne, 26. (Gazzetta dello Sport)

Habari zilizothibitishwa tutakujuza mara zitakapothibitishwa. Kwa orodha kamili ya wachezaji waliokamilisha rasmi usajili bofya link hii: http://www.bbc.co.uk/sport/football/transfers

Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa. Uwe na wiki njema.