Marekani: Vita vya Korea Kaskazini vitakuwa vya kutamausha

North Korean leader Kim Jong-Un inspects the Command of the Strategic Force of the Korean People"s Army Haki miliki ya picha AFP PHOTO/KCNA VIA KNS
Image caption Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un

Hatua za kijeshi dhidi ya Korea Kaskazini zitakuwa za kutamausha, lakini kuna uwezekano wa hatua hiyo kuchukuliwa, mshauri mkuu wa kijeshi wa Rais Donald Trump amesema.

Gen Joseph Dunford, mwenyekiti ya makanda ya kikosi cha pamoja cha Marekani alitoa matamshi hayo akifanya ziara nchini China.

Alikuwa akijibu matamshi ya msaidizi mku wa Trump, aliyetupilia mbalia hatau za kijeshi dhidi ya mpango wa nyuklia wa Korea Kaskazini.

Misukosuko imekuwa ikiongezeka kati ya Marekani na Korea Kaskazini baada ya Korea kupiga hatua kati majaribio yake ya makombora.

Trump ameionya Korea Kaskazini kuwa itakabiliwa vikali huku nayo Korea Kaskazini ikionya kuwa itashambulia himaya ya Marekani ya Guam.

Lakini majibizano makali ya wiki iliyopita yamepoa baada kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un kusitisha mpanao wa kuishambulia Guam.

"Trump ametuambia kuandaa mipango mwafaka ya kijeshi, na hilo ndilo tunafanya kwa sasa." Gen Joseph Dunford alisema.

Afisa wa cheo cha juu wa jeshi la China ambaye alikutana na Gen Dunford, aliamua kuwa hatua za kijeshi hazistahili na kwamba mazungumzo ndio njia pekee.

China ndiyo mshirika wa peke wa Korea Kaskazini.

Mada zinazohusiana