Zaidi ya watu 40 wauwawa kwenye maporomoko ya ardhi DRC

Zaidi ya watu 40 wameuawa kwenye janga la maporomoko ya ardhi kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Demokrasi ya Congo.

Wengi wa wale waliouawa ni kutoka kijiji kimoja kinachofanya uvuvi katika kingo za ziwa Albert.

Mvua kubwa imesababisha sehemu za mlima ulio karibu kuporomoka na kufunika kijiji hicho kwa mujibu wa shirika la habari la AFP.

Watu wengine kadhaa walifariki wakitafuta dhahabu kwenye migodi ya zamani.

Kumekuwa na majanga mabaya ya maporomo ya ardhi mashariki mwa Jamhuri ya Demokrasi ya Congo miaka ya hivi karibuni.

Janga hili linatokea baada ya mafuriko mabaya yaliyotekea kwenye mji wa Freetown nchini Sierra Leone siku ya Jumatatu ambapo zaidi ya watu 300 waliuawa.

Ripoti zinasema kuwa watu 28 walizikwa jana huku 12 wengine wamezikwa leo.

Mada zinazohusiana