Watu 13 wauawa na mamia kujeruhiwa, Barcelona

Huwezi kusikiliza tena
Gari lagonga watu eneo la watalii mjini Barcelona

Serikali ya Catalonia imesema watu 13 wamekufa na wengine zaidi ya 100 kujeruhiwa baada ya gari la mizigo kugonga watu katika eneo la watalii la Las Ramblas, Barcelona.

Polisi nchini Uhispania wanasema kuwa watu kadhaa wamejeruhiw watoa huduma za dharura wakiwashauri watu kukaa mbali na eneo hilo.

Ripoti kutoka eneo hilo zinasema kuwa watu wanajificha ndani ya maduka yaliyo karibu.

Shirika la hahari la Reuters linasema kuwa watoa huduma za dharura wameomba kusitishwa kwa huduma za usafiri wa mabasi na kufungwa vituo vya treni.

Gazeti la El Pais lilisema kuwa dereva wa gari aliliendesha na kutoroka kwa miguu baada ya kuwagonga watu kadha.

Image caption Shirika la hahari la Reuters linasema kuwa watoa huduma za dharura wameomba kusitishwa kwa huduma za usafiri wa mabasi na vituo vya treni.

"Watu kwenye ofisi yangu waliona gari likiendeshwa kwenda kwa umati wa watu huko Las Ramblas," alisema mtu moja anayefanya kazi sehemu hiyo.

"Niliona karibu watu wawili au watatu hivi wakilala chini.

"Kuna magari kadha ya kubeba wagonjwa na polisi waliojihami wakiwa na bunduki kwa sasa," alisema.

Taarifa za kina kuhusu kisa hiki bado hazipo lakini magari yashatumiwa kugonga watu kwenye misururu ya mashambulizi barani Ulaya tangu mwezi Julai mwaka uliopita.

Mada zinazohusiana