Marekani yazidi kuionya Korea Kaskazini

Kiongozi wa Korea kaskazini Haki miliki ya picha AFP
Image caption Kiongozi wa Korea kaskazini

Waziri wa Ulinzi wa Marekani James Mattis ameionya Korea Kaskazini kuchukuliwa hatua kali za kijeshi, iwapo itaanzisha uadui.

Amesema majibu ya hayo itakuwa ni maangamizi, lakini pia ameitaka Korea kaskazini kuepuka uchokozi.

Mafisa wa Marekani na Japan wamesema wataongeza ushirikiano wao wa kiulinzi kuweza kupambana na kitisho cha nyuklia cha Korea kaskazini.

Wizara ya Ulinzi ya Marekani Pentagon imetangaza kwamba jenerali Mattis na mashirika wake wa Korea Kusini , Waziri wa Ulinzi Song Young-moo watakutana baadaye mwezi huu.

Marekani pia imesisitiza kuendelea na mafunzo ya kijeshi wanayofanya kwa ushirikiano na Korea kusini wiki ijayo, licha ya shinikizo wanazopata kutoka China na Korea kaskazini kutaka waachane na jambo hilo.