Matokeo kufuzu klabu bingwa Ulaya.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption AC Milan

AC Milan wamewapiga bao 6 Shkendija kutoka Macedonia.

Andre Silva ambaye AC Milan wamemnunua kutoka Porto amefunga mawili.

Fabio Borini aliyechukuliwa kwa mkopo kutoka Sunderland pia amefunga goli lake la kwanza, Luca Antonelli na Riccardo Montolivo nao pia wamezifumania nyavu.

Mara ya mwisho AC Milan kutoa kichapo kikali kama hiki nyumbani ilikuwa ushindi wake wa bao 8 dhidi ya Union Luxembourg msimu ule wa mwaka 1962- 63.