Watalii kutoka China watembelea Mogadishu

Watalii kutoka China watembelea Mogadishu
Maelezo ya picha,

Watalii kutoka China watembelea Mogadishu

Kundi moja la Wachina 27 limeondoka mjini Mogadishu nchini Somalia baada ya ziara ya siku kadhaa .

Maafisa kutoka wizara ya Utalii mjini Mogadishu wamesema kuwa serikali iliwaandaa watalii hao katika maeneo tofauti ya Mogadishu.

Hatahivyo vyombo vya habari na wakaazi walijua habari hiyo baada ya wao kuondoka nchini.

Sio swala la kawaida kuwa na watalii nchini Somalia tangu taifa hilo la pembe ya Afrika kukumbwa na mgogoro yapata miongo miwili iliopita.

Sasa inaonekana kwamba watalii hao wa China ambao wameuwa mjini Mogadishu kwa siku kadhaa waliondoka.

Habari hiyo ilifichwa kutoka kwa wanahabari hadi walipoondoka kutokana na swala la utovu wa usalama nchini humo.

Afisa mmoja wa serikali amesema kuwa wanatarajia watalii zaidi kutembelea taifa hilo

Kuna wafanyikazi wengi wa kimataifa nchini Somalia wakiwemo wale wa Uturuki, Kenya pamoja na wale wa mataifa ya magharibi