Picha za Afrika wiki hii: 11 - 17 Agosti 2017

Baadhi ya picha zilizovutia kutoka Afrika na za Waafrika wakiwa mahala tofauti ulimwenguni wiki hii.

Wanafunzi bora zaidi nchini Ivory Coast walialikwa kwenye ikulu ya rais, mji mkuu Abidjan, ikiwa ni pamoja na msichana huyu aliyepigwa picha kwenye dawati la makamu wa rais siku ya Ijumaa. Alikuwa kati ya wanafunzi 51 waliotuzwa kwa kupata alama za juu darasani katika mitihani wa mwisho wa mwaka. Haki miliki ya picha AFP

Wanafunzi bora zaidi nchini Ivory Coast walialikwa kwenye ikulu ya rais, mji mkuu Abidjan, ikiwa ni pamoja na msichana huyu aliyepigwa picha kwenye dawati la makamu wa rais siku ya Ijumaa. Alikuwa kati ya wanafunzi 51 waliotuzwa kwa kupata alama za juu darasani katika mitihani wa mwisho wa mwaka.

Jumapili, Mji mkuu wa Tunisia, Tunis, wanawake wanapigwa picha wakiwa wamevalia ma vazi ya kitamaduni inayojulikana kama Sefseri, wakati wa sherehe ya Siku ya Wanawake. Haki miliki ya picha EPA

Jumapili, Mji mkuu wa Tunisia, Tunis, wanawake wanapigwa picha wakiwa wamevalia mavazi ya kitamaduni inayojulikana kama Sefseri, wakati wa sherehe ya Siku ya Wanawake.

Siku ya jumanne Wizara ya mambo ya kale nchini Misri ilitoa picha mpya ya vitu vilivyovumbuliwa majuzi, ikiwa ni pamoja na sanamu hii iliyopatikana eneo la Minya karibu na mto Nile. Waakiolojia wanaamini kuwa makaburi hayo ni ya nyakati ya nasaba ya 27 ya Misri na zama za Kigiriki na Kirumi. Haki miliki ya picha EPA

Siku ya jumanne Wizara ya mambo ya kale nchini Misri ilitoa picha mpya ya vitu vilivyovumbuliwa majuzi, ikiwa ni pamoja na sanamu hii iliyopatikana eneo la Minya karibu na mto Nile. Waakiolojia wanaamini kuwa makaburi hayo ni ya nyakati ya nasaba ya 27 ya Misri na zama za Kigiriki na Kirumi.

Timu ya wanaume ya Botswana ya mbio za kupokezana vijiti za 4x400m ilikosa nafasi ya kushiriki katika fainali kwenye michuano ya Dunia mjini London siku ya Jumamosi, baada ya who kuangushja kijiti. Kosa lililowaacha katika nafasi ya saba. Haki miliki ya picha Reuters

Timu ya wanaume ya Botswana ya mbio za kupokezana vijiti za 4x400m ilikosa nafasi ya kushiriki katika fainali kwenye michuano ya dunia mjini London siku ya Jumamosi, baada ya wao kuangusha kijiti. Kosa lililowaacha katika nafasi ya saba.

Siku ya Ijumaa, wafuasi wa chama cha Jubilee nchini Kenya waanza kusherehekea wakisubiri Rais Uhuru Kenyatta atangazwe mshindi wa uchaguzi mkuu. Uhuru alishinda na asilimia 54 za kura dhidi ya mpinzani wake Raila Odinga, aliyepata asilimia 45. Haki miliki ya picha EPA

Siku ya Ijumaa, wafuasi wa chama cha Jubilee nchini Kenya waanza kusherehekea wakisubiri Rais Uhuru Kenyatta atangazwe mshindi wa uchaguzi mkuu. Uhuru alishinda na asilimia 54 za kura dhidi ya mpinzani wake Raila Odinga, aliyepata asilimia 45.

Siku mbili baadaye, Raila Odinga ambaye alikataa kukubali matokeo ya kura za urais anaonekana mtaa wa Mathare jijini Nairobi, ambako ni ngome ya upinzani. Baadaye alitangaza kuwa atakwenda mahakamani kupinga matokeo ya uchaguzi. Haki miliki ya picha AFP

Siku mbili baadaye, Raila Odinga ambaye alikataa kukubali matokeo ya kura za urais anaonekana mtaa wa Mathare jijini Nairobi, ambako ni ngome ya upinzani. Baadaye alitangaza kuwa atakwenda mahakamani kupinga matokeo ya uchaguzi.

Eva Msando, mjane wa Chris Msando katika misa ya wafu jijini Nairobi tarehe 17 Agosti 2017. Haki miliki ya picha Roderick MaCleod/BBC

Mjane wa aliyekuwa mfanyikazi wa tume ya uchaguzi ya Kenya aliyeuawa Chris Msando akihudhuria misa ya wafu ya mume wake siku ya Alhamisi, pamoja na mtoto wao mdogo. Uchunguzi kuhusu kifo cha Msando, ambaye alikuwa mmoja wa waliofahamu mfumo wa kidijitali wa kupiga kura na aliyeuawa siku chache tu kabla ya uchaguzi mkuu, unaendelea.

Waandamanaji wanajipiga picha Jumatatu mjini London kama njia ya kukashifu kukamatwa na kuzuiliwa kwa mpiga picha Mahmoud Abu Zeid . Amezuiliwa tangu mwaka wa 2013 kwa kupiga picha wakati wa operesheni ya kijeshi, na kuna hofu anaweza kuhukumiwa kifo. Haki miliki ya picha Reuters

Waandamanaji wanajipiga picha Jumatatu mjini London kama njia ya kukashifu kukamatwa na kuzuiliwa kwa mpiga picha Mahmoud Abu Zeid . Amezuiliwa tangu mwaka wa 2013 kwa kupiga picha wakati wa operesheni ya kijeshi, na kuna hofu anaweza kuhukumiwa kifo.

Ganiyu Oyinlola ni mshonaji nguo katika wilaya ya Ikeja, jijini Lagos. Amepigwa picha akishona vazi la mteja siku ya Jumamosi. Haki miliki ya picha Reuters

Ganiyu Oyinlola ni mshonaji nguo katika wilaya ya Ikeja, jijini Lagos. Amepigwa picha akishona vazi la mteja siku ya Jumamosi.

Gabriella Engels, ambaye anadai kudhulumiwa na mke wa Rais wa Zimbabwe Grace Mugabe, akiwa na wanahabari siku ya Alhamisi. Ameiambia BBC kuwa anaogopa maisha yake yamo hatarini. Haki miliki ya picha Reuters

Gabriella Engels, ambaye anadai kudhulumiwa na mke wa Rais wa Zimbabwe Grace Mugabe, akiwa na wanahabari siku ya Alhamisi. Ameiambia BBC kuwa anaogopa maisha yake yamo hatarini.

Kaburi zinachimbwa katika makaburi ya Paloko, eneo la Waterloo, Sierra Leone Agost i17, 2017. Haki miliki ya picha Reuters

Mazishi ya watu 400, katika kaburi la wengi yanaendelea nje ya Freetown, Sierra Leone, siku ya Alhamisi. Takriban watu 600 bado hawajulikani waliko tangu maporomoko ya udongo kutokea Jumatatu. Watu wengine takriban elfu tatu wameachwa bila makao.

Mama huyu aliyepoteza mtoto wake kwenye mkasa huo anaomboleza nje ya hospital siku moja kabla ya kuutambua mwili wake. Haki miliki ya picha Reuters

Mama huyu aliyepoteza mtoto wake kwenye mkasa huo anaomboleza nje ya hospital siku moja kabla ya kuutambua mwili wake.

Mtoto anawatazama walinda amani wa Umoja wa Mataifa wakati wa ziara ya kamishna mkuu wa UN katika kambi ya wakimbizi ya Al-Nimir nchini Sudan, ambako ni nyumbani kwa wakimbizi zaidi ya 5,000 wa Sudan Kusini. Wengi wa wale wanaokimbia vita katika nchi zao husafiri Uganda, ambayo hadi sasa imekaribisha wakimbizi milioni moja kutoka Sudan Kusini. Haki miliki ya picha AFP

Mtoto anawatazama walinda amani wa Umoja wa Mataifa wakati wa ziara ya kamishna mkuu wa UN katika kambi ya wakimbizi ya Al-Nimir nchini Sudan, ambako ni nyumbani kwa wakimbizi zaidi ya 5,000 wa Sudan Kusini. Wengi wa wale wanaokimbia vita katika nchi zao husafiri Uganda, ambayo hadi sasa imekaribisha wakimbizi milioni moja kutoka Sudan Kusini.

Picha ni kwa hisani ya AFP, EPA, Getty Images na Reuters