Iraq yafanya mashambulizi ya ardhini kuuteka mji wa Tal Afar kutoka IS

Iraqi armoured vehicles are transported to the frontline outside Tal Afar (15 August 2017 Haki miliki ya picha AFP
Image caption Iraq yafanya mashambulizi ya ardhini kuuteka mji wa Tal Afar kutoka IS

Wanajeshi wa Iraq na makundi ya wapiganaji yanaounga serikali mkono wameanza mashambulizi ya ardhini katika mji wa Tal Afar, mojawepo wa ngome zilizosalia mikononi mwa kundi la kigaidi la Islamic state.

Mji huo umekuwa chini ya udhibiti wa Islamic state tangu mwaka 2014.

Akihutubia taifa kupitia runinga,waziri mkuu Haider al-Abadi, amesema wapiganaji wa Islamic state huko Tal Afar wanafaa kujisalimisha ama wauwawe.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Wapiganaji wa kiShia

Takriban wapiganaji 2000 wa Islamic state wanaaminika kuwa wamesalia katika mji huo, ambao umezingirwa tangu mwezi Juni, na umekuwa ukishambuliwa kutoka angani na ndege za kivita za Marekani na Iraq.

Raia Wengi walitoroka mji huo, japo 40,000 walibaki.

Ndege za jeshi la Iraq zimeshambulia ngome za IS katika mji huo kwa siku kadha, kuandaa mashambulizi ya ardhini

Image caption Iraq yafanya mashambulizi ya ardhini kuuteka mji wa Tal Afar kutoka IS