Washambuliaji wa Barcelona walipanga kutumia mitungi 120 kwa mashambulizi ya kigaidi

Police say the destroyed house in Alcanar is a focal point of the investigation Haki miliki ya picha EPA
Image caption Washambuliaji wa Barcelona walikuwa na mitungi 120 kufanyia mashambulizi

Washukiwa wa ugaidi ambao waliendesha mashambulilizi nchini Uhispania walikuwa wamekusanya mitungi 120 na walikuwa wakipanga kuitumia kwenye mashambulizi ya magari, kwa mujibu wa polisi nchini Uhispania.

Mitungi hiyo ilipatikana ndani ya nyumba ambayo inadaiwa kutumiwa na magaidi hao katika mji wa Alcanar siku ya Jumatano usiku.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Washambuliaji wa Barcelona walikuwa na mitungi 120 kufanyia mashambulizi

Polisi bado wanamtafuta dereva wa gari ambalo liligonga watu kadha katika eneo la Las Ramblas mjini Barcelona na kuwaua 13.

Leo Jumapili misa ilifanyika mjini Barcelona kuwaomboleza waathiriwa.

Kando na watu 13 waliouawa siku ya Alhamisi huko Las Ramblas, mwanamke mwingine aliuawa wakati wa shambulizi la pili la gari mapema Ijumaa katika mji wa Cambrils.

Image caption Washambuliaji wa Barcelona walikuwa na mitungi 120 kufanyia mashambulizi

Washukiwa watano magaidi waliuawa kwa kupigwa risasi kwenye shambuliza hilo la pili.

Polisi wamethibitisha kuwa bado wanamsaka Younes Abouyaaqoub, mzaliwa wa Morocco, kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Uhispania.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption (kutoka kushoto) Moussa Oukabir, Said Aallaa, Mohamed Hychami na Younes Abouyaaqoub

Mada zinazohusiana