Manowari ya Marekani yagongana na meli ya mafuta pwani mwa Singapore

Manowari ya Marekani yagongana na meli ya mafuta pwani mwa Singapore Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Manowari ya Marekani yagongana na meli ya mafuta pwani mwa Singapore

Wanajeshi 10 hawajulikani waliko na wengine watano wamejeruhiwa baada ya manowari ya jeshi la Marekani kugongana na meli ya kubeba mafuta pwani mwa Singapore, kwa mujibu wa jeshi la wanamaji la Marekani.

Manowari ya USS John MacCain ilikuwa mashariki mwa Singapore ikijiandaa kutia nanga bandarini wakati iligongana na meli iliyokuwa ikipeperusha bendera ya Liberia.

Shughuli kubwa ya kuwatafuta na kuwaokoa wanajeshi inaendelea.

Ndicho kisa cha pili kikubwa kinachoikumba meli ya jeshi la wanamaji wa Marekani miezi ya hivi karibuni.

Ripoti zinasema kuwa manowari hiyo ilikumbwa na uharibifu upande wake mmoja, lakini jeshi la Marekani lilsema kwa inaelea peke yake kwenda bandari ya Singapore.

Helikopta za jeshi la Marekani na jeshi la Singapore pamoja na walinzi wa pwani, wanafanya shughuli za uokoaji. Malaysia nayo imejiunga katika shughuli hiyo.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Manowari ya Marekani yagongana na meli ya mafuta pwani mwa Singapore

Kisa hiki kinatokea siku ya kwanza ya mazoezi ya kila mwaka ya kijeshi kati ya jeshi la Marekani na Korea Kaskazini, ishara ya ubabe wa kijeshi dhidi ya Korea Kaskazini.

USS John Mccain ni moja ya manowari saba za Marekani zinazoshiriki, lakini kisa hiki kitachangia kuwepo maswali kuhusu shughuli za jeshi la wanamaji eneo hilo.

Hiki ndicho kikosi kile kile ambacho kilikumbwa na ajali mwezi Juni, wakati wanajeshi 7 wa Marekania waliuawa. Ni wiki iliyopita tu ambapo maafisa saba waliadhibiwa kufuatia kisa hicho.

Image caption Manowari ya USS John MacCain ilikuwa mashariki mwa Singapore ikijiandaa kutia nanga bandarini

Hii pia inatajwa kuwa mkasa wa nne wa kugongana kwa meli za jeshi la Mareknia mwaka hu pekee.

Kuna taarifa kidogo kuhusu hali ya meli ya mafuta ya Alnic MC na wahudumu wake.

Meli hiyo ya mafuta inaripotiwa kuwa na uzito mara tatu zaidi na wa manowari ya jeshi ya USS John McCain, na taarifa zinasema kuwa haikuwa imebeba mafuta wakati ya ajali hiyo.

Seneta John McCain ambaye jina lake limepewa manowari hiyo, aliandika kwenye mtandao wa twitter kuwa yeye na mke wake wanawaombea mabaharia hao.

Mwezi Juni mabaharia saba wa Marekani waliuawa wakati manowari ya USS Fitzgerald iligongana na meli ya mizigo kwenye bahari ya Japan karibu na bandari ya Yokosuka.

Mada zinazohusiana