Shughuli ya kumwinda dereva aliyeua watu Barcelona yapelekwa kote Ulaya

A set of three images showing a figure wearing sunglasses walking through Barcelona's streets Haki miliki ya picha El Pais
Image caption Video mpya za CCTV zinaoneonekana kumuonyesha akikimbia eneo la shambulizi kwa miguu.

Shughulia la kumwinda dereva ambaye aliwaua watu 13 wiki iliyopita mjini Barcelona imepelekwa kote Ulaya.

Polisi wanasema kuwa kwa sasa wamemtambua dereva huyo lakini hawakumtaja jina lake.

Lakini afisa mmoja aliiambia radio moja kuwa kila kitu kinaonyesha kuwa dereva huyo ni Younes Abouyaaqoub.

Mamlaka zinasema kuwa haziwezi kukana kuwa huenda amevuka mpaka na kuingia nchini Ufaransa.

Video mpya za CCTV zinaoneonekana kumuonyesha akikimbia eneo la shambulizi kwa miguu.

Haki miliki ya picha AFP/Getty
Image caption Polisi wanasema wanachuguza uwezekano kuwa dakika 90 baadaye Younes Abouyaaqoub alimchoma kisu na kumuua mwanamume mmoja na kuiba gari lake.

Picha tatu kwenye gazeti la El Pais zinadaiwa kuonyeha mwanamume huyo akitembea kupitia soko la La Boqueria aliwa amevaa miwani.

Polisi wanasema wanachuguza uwezekano kuwa dakika 90 baadaye, alimchoma kisu na kumuua mwanamume mmoja na kuiba gari lake.

Jana afisa mkuu wa polisi huko Catalan Josep Lluis Trapero alisema kuwa kati ya washukiwa 12, ni mmoja tu ambaye anadiwa kuwa Abouyaaqoub hajakamatwa.

Wanne wamekamatwa na kuna miili miwili ambayo hiajatambuliwa. Washukiwa watano waliuawa wakati wa shambulizi la pili huko Cambrils.

Mada zinazohusiana