Jua litapatwa lini tena nchini mwako?

Total Solar Eclipse Haki miliki ya picha Getty Images

Jumatatu 21 Agosti 2017 mamilioni ya Wamarekani watashuhudia moja ya tukio kubwa zaidi ya jua kupatwa na mwezi katika kipindi cha karibu miaka 100.

Kwa kawaida, jua hupatwa mara mbili hivi kila mwaka, na hilo hutokea njia inayofuatwa na Jua, Dunia na Mwezi huendana sambamba.

Hili hapa ni jedwali la kuonesha ni lini mataifa mbalimbali Afrika yatashuhudia jua likipatwa hivi akribuni.

Takwimu zimetoka kwa Shirika la Anga za Juu la Marekani.

Kupatwa kwa jua kikamilifu 21 Agosti

Jua litapatwa kikamilifu leo kuanzia maeneo ya kaskazini mashariki mwa Bahari ya Pasifiki kabla ya kuanza kuonekana ardhini katika Lincoln Beach, Oregon mwendo wa saa 10:16 saa za huko (18:16 BST/Saa mbili jioni Afrika Mashariki).

Ukanda ambapo kutakuwa na giza totoro utapitia Amerika Kaskazini kwa dakika 90 hivi na kupitia maeneo ya Oregon, Idaho, Wyoming, Nebraska, Missouri, Illinois, Kentucky, Tennessee, North Carolina, South Carolina na Georgia.

Majimbo mengine nchini Canada na mataifa mengine ya Amerika Kusini na Kati pia yatashuhudia kupatwa kwa jua kisehemu.

Aidha, baadhi ya nchi za Afrika Magharibi na Ulaya magharibi pia zitashuhudia kupatwa kwa jua kisehemu. Lakini nchini Uingereza, katika maeneo mengi, jua litazibwa asilimia 4 pekee mwendo wa saa 20:00 BST.

Jua hupatwa vipi?

Kupatwa kwa jua kunatokea wakati dunia, mwezi na jua vinapokaa kwenye mstari mmoja mnyoofu wakati mwezi unakuwa kati ya dunia na jua. Hali hiyo inapotokea huwa kunajengeka kivuli cha mwezi kwenye uso wa dunia.

Kivuli hicho hufunika sehemu tu ya uso wa dunia.

Kutokana na hali hiyo kupatwa kwa jua kwa maeneo yaliyo mengi huwa kunaonekana kwa watu wengi kama kupungua kwa mwanga wa jua.

Hili hutokea takriban mara moja kila mwezi, lakini kutokana na mwinambo wa njia inayofuatwa na mwezi huwa hili linatokea juu sana au chini sana kwenye mbingu kiasi kwamba huwa haliwezi kuziba mwanga wa jua.

Sehemu yenye giza zaidi hufahamika kama kivuli cha kati na hapa ndipo jua hupatwa kikamilifu.

Sehemu ya nje hufahamika kama kivuli cha kando, ambapo jua huwa mwanga wake umezibwa kiasi tu. Hili husababisha kupatwa kwa jua kisehemu.

Kupatwa kwa jua kipete ni hali inayotokea ambapo mwezi huzuia mwanga wa jua kufika kwenye dunia kwa vile huweka duara la kivuli cha mwezi kwenye dunia na hivyo mwanga wa jua huonekana kama pete.

Aina hii ndiyo iliyoshuhudiwa nchini Tanzania tarehe 1 Septemba 2016 na katika baadhi ya maeneo ya bara la Afrika.

Taifa Tarehe Aina ya kupatwa kwa jua
Algeria 6/21/2020 Kupatwa kwa jua kipete
Angola 6/21/2020 Kupatwa kwa jua kipete
Benin 6/21/2020 Kupatwa kwa jua kipete
Botswana 6/21/2020 Kupatwa kwa jua kipete
Burkina Faso 6/21/2020 Kupatwa kwa jua kipete
Burundi 6/21/2020 Kupatwa kwa jua kipete
Capo Verde 10/14/2023 Kupatwa kwa jua kipete
Cameroon 6/21/2020 Kupatwa kwa jua kipete
Jamhuri ya Afrika ya Kati 6/21/2020 Kupatwa kwa jua kipete
Chad 6/21/2020 Kupatwa kwa jua kipete
Comoros 6/21/2020 Kupatwa kwa jua kipete
Congo (DR) 12/26/2019 Kupatwa kwa jua kipete
Congo 6/21/2020 Kupatwa kwa jua kipete
Cote d'Ivoire 12/14/2020 Kupatwa kwa jua kikamilifu
Djibouti 12/26/2019 Kupatwa kwa jua kipete
Egypt 12/26/2019 Kupatwa kwa jua kipete
Equatorial Guinea 6/21/2020 Kupatwa kwa jua kipete
Eritrea 12/26/2019 Kupatwa kwa jua kipete
Ethiopia 12/26/2019 Kupatwa kwa jua kipete
Gabon 6/21/2020 Kupatwa kwa jua kipete
Gambia, The 10/14/2023 Kupatwa kwa jua kipete
Ghana 6/21/2020 Kupatwa kwa jua kipete
Guinea 10/14/2023 Kupatwa kwa jua kipete
Guinea-Bissau 10/14/2023 Kupatwa kwa jua kipete
Kenya 12/26/2019 Kupatwa kwa jua kipete
Liberia 2026-12-08T00:00:00.000 Kupatwa kwa jua kikamilifu
Libya 6/21/2020 Kupatwa kwa jua kipete
Madagascar 6/21/2020 Kupatwa kwa jua kipete
Malawi 6/21/2020 Kupatwa kwa jua kipete
Mali 6/21/2020 Kupatwa kwa jua kipete
Mauritania 6/21/2020 Kupatwa kwa jua kipete
Mauritius 2/17/2026 Kupatwa kwa jua kipete
Morocco 6/21/2020 Kupatwa kwa jua kipete
Msumbiji 6/21/2020 Kupatwa kwa jua kipete
Namibia 6/21/2020 Kupatwa kwa jua kipete
Niger 6/21/2020 Kupatwa kwa jua kipete
Nigeria 6/21/2020 Kupatwa kwa jua kipete
Rwanda 6/21/2020 Kupatwa kwa jua kipete
Senegal 10/14/2023 Kupatwa kwa jua kipete
Seychelles 6/21/2020 Kupatwa kwa jua kipete
Sierra Leone 10/14/2023 Kupatwa kwa jua kipete
Somalia 12/26/2019 Kupatwa kwa jua kipete
Afrika Kusini 6/21/2020 Kupatwa kwa jua kipete
Sudan Kusini 12/26/2019 Kupatwa kwa jua kipete
Sudan 12/26/2019 Kupatwa kwa jua kipete
Swaziland 6/21/2020 Kupatwa kwa jua kipete
Tanzania 12/26/2019 Kupatwa kwa jua kipete
Tunisia 6/21/2020 Kupatwa kwa jua kipete
Uganda 12/26/2019 Kupatwa kwa jua kipete
Zimbabwe 6/21/2020 Kupatwa kwa jua kipete

Mada zinazohusiana