Mtu mmoja auawa baada ya gari kugonga kituo cha basi Ufaransa

Site of bus stop death in Marseille Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mtu mmoja auawa baada ya gari kugonga kituo cha basi Ufaransa

Mtu moja ameuawa baada ya gari kugonga kibanda cha kituo cha mabasi kwenye mji ulio kusini mwa Ufaransa wa Marseille.

Dereva wa gari hilo amekatwa. Polisi wanasema kuwa haijulikani ikiwa gari hilo liliendeshwa makusudi kwenda kwa kibanda hicho au ni ajali ya kawadia.

Lakini kuna ripoti kuwa kibanda kingine cha kituo cha mabasi kwenye wiliya tofaua kiligongwa mapema.

Polisi wamewashauri watu kuchukua tahadhari.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mtu mmoja auawa baada ya gari kugonga kituo cha basi Ufaransa

Vyombo vya habari nchini Ufaransa vinasema kuwa mwanamke ambaye aliuawa alikuwa wa umri wa miaka 40 hivi na dereva alikuwa mwanamume wa miaka 35 na alikuwa akifahamika kwa polisi.

Hakuna taarifa kamili kuhusu lengo ya kisa hicho.

Mwaka uliopita mjini Nice, zaidi ya watu 80 waliuawa wakati lori liliendeshwa kwenda kwa umati uliokuwa ukisherehekea, shambulizi ambalo Islamic State ilidai kutekeleza.

Mada zinazohusiana