Tanzania kutumia sanaa kukabiliana na rushwa

Tanzania imekuwa ikiendesha kampeni ya kukabiliana na rushwa Haki miliki ya picha PCCP/Tanzania
Image caption Tanzania imekuwa ikiendesha kampeni ya kukabiliana na rushwa

Tanzania kupitia makumbusho ya Taifa imenza kampeni rasmi ya kupinga rushwa kwa kutumia sanaa ya uchongaji na jukwaani.

Tanzania ambayo kwa mujibu wa shirika la Transparency International mwaka 2016 ilikuwa ya 116 katika orodha ya viwango vya rushwa duniani miongoni mwa mataifa 176.

Sudan Kusini na Somalia zilishikilia nafasi za mwisho, 172 na 176 mtawalia kwenye orodha hiyo.

Sanaa hizo zitahusisha vinyago, michoro na maigizo yenye dhima ya kuonyesha mazingira ya rushwa za aina mbalimbali katika jamii na namna ya kukabiliana nayo.

Mbinu hii itatumika katika matamasha ya wazi ambayo yanatarajiwa kuanza kufanyika mwishoni mwa mwezi Agosti jijini Dar es salaam na kuendelea katika baadhi ya mikoa nchini humo.

Mada zinazohusiana