Urusi yashutumu vikwazo vya Marekani kuhusu viza

St Petersburg Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Uhasama kati ya Marekani na Urusi kwa sasa umelinganishwa na hali ya kutoaminiana wakati wa Vita Baridi

Urusi imeshutumu hatua ya Marekani ya kuamua kwamba ni lazima raia wa Urusi wanaotaka kuzuru Marekani wawe wakienda Moscow kuomba viza.

Taarifa kutoka ubalozi wa Marekani nchini humo imesema viza za raia wa Marekani hazitakuwa zikishughulikiwa tena katika afisi tatu za kibalozi za Marekani nchini Urusi.

Hilo litafanyika katika ubalozi mjini Moscow pekee.

Waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergei Lavrov amesema hilo ni jaribio la kuwachochea raia wa Urusi dhidi ya serikali yao wenyewe.

Mwezi uliopita, Moscow iliiagiza Marekani kuondoa maafisa 755 kutoka kwenye idadi ya maafisa katika ubalozi wake nchini humo.

Ubalozi wa Marekani ulisema kwamba kuhusiana na hatua ya Urusi kupunguza idadi ya wafanyakazi katika afisi za kibalozi nchini humo hadi 455, afisi za kibalozi nchini Urusi zitaacha kutoa viza kwa raia wa Urusi kwa muda usiojulikana kuanzia 23 Agosti.

Marekani ina afisi za kibalozi katika miji ya St Petersburg, Yekaterinburg and Vladivostok.

Wengi wa wafanyakazi 755 wa Marekani watakaoachishwa kazi ni wenyeji na hivyo basi hawatahitaji akuondoka urusi.

Kremlin imesema imekuwa tu inaiambia Marekani kwamba iwe na wafanyakazi kiasi sawa na wale wa Urusi nchini Marekani.

Kumekuwa na mgogoro wa kidiplomasia kati ya Urusi na Marekani tangu Urusi ilipotwaa rasi ya Crimea kutoka wka Ukraine mwaka 2014.

Alipokuwa akishutumu hatua hiyo, Bw Lavrov amesema Urusi haitalipiza kisasi hatua hiyo kwa Wamarekani wanaoomba viza za Urusi.

Bw Lavrov amesema hatua hiyo ni juhudi za kufanikisha mapinduzi, juhudi zilizoanza wakati wa Obama.

Mtangulizi wa Donald Trump, Barack Obama, aliwafungia wanabalozi 35 kuingia Marekani Desemba kuhusiana na tuhuma kwamba Urusi iliingilia uchaguzi wa Marekani kufaa upande wa Trump.

Hatua ya Lavrov kugusia mapinduzi imeonesha imani ya Kremlin kwamba uingiliaji wa Marekani ulichochea mapinduzi nchini Georgia mwaka 2003 na mapinduzi ya Ukraine mwaka 2004, mataifa ya zamani ya Muungano wa Usovieti.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii