Upinzani wasema maandamano yalisababisha vifo Togo

Maandamano hayo yalikuwa kwa ajili ya kuupinga utawala wa Rais Faure Gnassingbé
Image caption Maandamano hayo yalikuwa kwa ajili ya kuupinga utawala wa Rais Faure Gnassingbé

Viongozi wa upinzani na wanaharakati wa haki za binaadam nchini Togo wametaka kuundwa kwa tume huru itakayochunguza mauaji ya watu wawili yaliyotokea wakati wa maandamano nchini humo.

Upinzani unasema kwamba watu saba waliuawa.

Serikali kwa upande wake inasema takriban maafisa sitini wa jeshi la polisi walijeruhiwa

Image caption Rais Faure Gnassingbé amekuwa madarakani tokea mwaka 2005

Upinzani nchini Togo uliitisha maandamano hayo ambayo yalitaka kufuatwa kwa katiba ya mwaka 1992 iliyoweka ukomo wa uongozi wa Rais.