Mwanajeshi mmarekani aliyeasi na kuhamia Korea Kaskazini mwaka 1962 afariki dunia

This handout taken in May 2005 and released on August 21, 2017 shows James Joseph Dresnok, a US defector to North Korea, in an unknown location. Haki miliki ya picha AFP / VeryMuchSo Productions
Image caption James Dresnok alifuka mpaka na kuingia Korea Kaskazini mwaka 1962

James Dresnok mwanejeshi wa mwisho wa Marekani anafahamika kuinshi nchini Korea Kaskanizi, alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 74 mwaka uliopita, kwa mjibu wa watoto wake.

Watoto wake Bw. Dresnok walisema kuwa alikuwa mtiifu kwa Korea Kaskazini hadi mwisho, kwenye mahojiano ya video iliyochapishwa wiki iliyopita.

Baada ya kuvuka na kuingia Korea Kaskazini mwaka 1962, alianza kuishi maisha yasiyo ya kawaida mjini Pyongyang.

Hi ni pamoja na kuibuka kwa nyota wa filamu katika sekta ya filamu nchini Korea Kaskazizi.

Uvumi kuhusu kifo cha bwana iliibuka mapema mwaka huu, na video ya hivi pude ya wanawe Ted na James Jr wakiwa wamevaa sare za jeshi na wakizungumza kwa ufasaha lugha ya kikorea

Haki miliki ya picha Uriminzokkiri
Image caption James Jr (kushoto)na Ted Dresnok wakiwa wamevaa sare za jeshi

"Kitu kimoja ambacho baba yetu alituomba tufanye ni tuwe wafanyakazi watiifu, kujitolea kwa kiongozi Kim Jong-Un na kuwalea watoto wetu waweze kufuata mwelekeo sawa na huo.

Video hiyo ilichapishwa na mtandao na shirika la habari la Korea Kaskazini la Uriminzokkiri wiki iliyopita.

Hii ni mara ya pili wanaume hao wawili wameonekana kwenye shirika hilo. Mwaka 2016 walionekana wakiisifu Korea Kaskazini kwenye kanda nyingine ya video.

Wote walisema kuwa wako kwebye jeshi la Korea Kaskanizini, wameoa na wana watoto.

Mada zinazohusiana