Polisi wawakamata wauaji wa wanawake Uganda

Inspekta jenerali wa polisi , Kale Kayihura Haki miliki ya picha ISAAC KASAMA
Image caption Inspekta jenerali wa polisi , Kale Kayihura

Maafisa wa polisi nchini Uganda wanasema kuwa wamewakamata washukiwa kadhaa kufuatia msururu wa mauaji ya wanawake karibu na miji mkuu wa Kampala.

Inspekta jenerali wa polisi , Kale Kayihura alisema kwamba mshukiwa mmoja amekiri kuwauawa wanawake wanane kufuatia agizo la mfanyibiashara mmoja.

Mauaji hayo yalikuwa ya tambiko fulani kulingana na jenerali Kayihura aliyewaambia wakaazi wa baraza la mji wa Nansana.

Vyombo vya habari vinasema wanawake 17 wameuawa katika hali ya kutisha tangu mwezi Mei.

Msemaji wa polisi Asan Kasingye aliambia BBC kwamba licha ya mauaji hayo kufanyika katika wilaya moja hayakuwa na uhusiano wowote.

Amesema kuwa katika kesi nyingi , waathiriwa walikuwa makahaba ambao walikuwa wamebakwa na kunyongwa katika maeneo yaliotengwa mida ya alfajiri.