Wahamiaji 20 wakamatwa kwa kusababisha fujo Ufaransa

Whamiaji wakiwa wamejipumzisha barabarani mjini Calais
Image caption Whamiaji wakiwa wamejipumzisha barabarani mjini Calais

Polisi mjini Calais nchini Ufaransa wamekamata watu 20 wanaotuhumiwa kuhusika kwenye fujo kati ya makundi mawili ya wahamiaji.

Takriban wahamiaji 150 kutoka Afghanistan na Eritrea walipigana katika mpaka wa Ufaransa na Uingereza.

Baadhi ya yao walijeruhiwa huku pia wakiharibu magari ya polisi kwa kuyapiga mawe.

Kambi ya wakimbizi ya Calais ilifungwa takriban mwaka mmoja uliopita, lakini ikafunguliwa kutokana na ongezeko la wahamiaji waliokuwa wakitarajia kuingia Uingereza.