Mamia wakusanyika kumsikiliza Trump Arizona

Trump amekuwa akipingwa kwa kutoa baadhi ya kauli zenye utata
Image caption Trump amekuwa akipingwa kwa kutoa baadhi ya kauli zenye utata

Mamia ya wafuasi wa Trump wamekusanyika katika mji wa Phoenix, Arizona kwa mkutano ambao utakaohutubiwa nae hivi punde.

Wapinzani wa Trump pia wamekusanyika kwa ajili ya kumpinga.

Meya wa mji huo awali alimtaka Trump achelewe kufika kwa madai ya kusababisha ubaguzi wa rangi nchini Marekani.

Image caption Kulikua na waliompinga pia katika mkutano huo

Ni kutokana na maneno ya Trump juu ya mgogoro ulioibuka kati ya weupe na weusi mapema mwezi huu mjini Charlottesville.