Kamanda wa kikosi cha majini cha Marekani kufutwa kazi baada ya manowari kugongwa

Vice Admiral Joseph Aucoin, U.S. 7th Fleet Commander, attends a media briefing on the status of the U.S. Navy destroyer USS Fitzgerald, damaged by colliding with a Philippine-flagged merchant vessel, and the seven missing Fitzgerald crew members, at the U.S. naval base in Yokosuka, south of Tokyo, Japan 18 June 2017. Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Joseph Aucoin alitarajiwa kustaafu wiki chache zinazokuja

Jeshi la wanamaji la Marekani limesema kuwa litamfuta kazi kamanda Joseph Aucoin wa kikosi cha wanamaji kinachofahamika kama Seventh Fleet, kufuatia visa vya kugongwa kwa manowari za kivita maeneo ya Asia.

Mabaharia 10 bado hawajulikani waliko baada ya manowari ya USS John S McCain kugongana na meli ya kubeba mafuta karibu Singapore siku ya Jumatatu.

Maafisa wa jeshi la wanamaji wanasema kuwa miili ya binadamu imepatikana ndani ya manowari hiyo ambayo kwa sasa imetia nanga katika bandari ya Singapore.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Manowari ya USS John S McCain ilikuwa mashariki mwa Singapore wakati iligongana na meli ya kubeba mafuta ya Alnic MC mapema siku ya Jumatatu.

Kisa hicho ndicho cha nne ya kugongwa kwa meli mwaka huu.

Kikosi cha Seventh Fleet chenye makao yake huko Yokosuka Japan kina karibu manowari 50 na 70 pamoja na nyambizi.

Joseph Aucoin ambaye amekuwa kamanda tangu mwaka 2015 alikuwa astaafu wiki chache zinazokuja,

Image caption Singapore

Kuondolewa kwake ni hatua ya hivi punde kuchukuliwa na maafisa wa jeshi la wanamaji baada ya kisa cha kugongwa kwa manowari ya USS John S McCain. Haijulianai ni lini tangazo rasmi litatolewa.

Manowari ya USS John S McCain ilikuwa mashariki mwa Singapore wakati iligongana na meli ya kubeba mafuta ya Alnic MC mapema siku ya Jumatatu.

Mada zinazohusiana