Trump aapa kuujenga ukuta wa Mexico

US President Donald Trump arrives to speak at a "Make America Great Again" rally in Phoenix, Arizona, on August 22, 2017 Haki miliki ya picha AFP
Image caption Trump anataka bunge la Congress kufadhili mpango wake wenye utata wa kujenga ukuta kati ya Marekani na Mexico ili kuwazuia wahamiaji haramu.

Donald Trump amesema kuwa atalizimika kuweka kando shughuli za serikali ikiwa itahitajika, ili aweze kujenga ukuta kwenye mpaka kati ya Marekani na Mexico.

Trump aliwaambia wafuasi wake kwenye mkutano uliofanyika huko Phoenix, Arizona, kuwa wabunge wa Democrats ndio kizuizi.

Wakati wa hotuba yake iliyochukua dakika 80, pia Trump alivilaumu vyombo vya hahari kwa kuwaunga mkono makundi yenye ubaguzi wa rangi nchini Marekani.

Trump anataka bunge la Congress kufadhili mpango wake wenye utata wa kujenga ukuta kati ya Marekani na Mexico ili kuwazuia wahamiaji haramu.

Lakini warepublican watahitaji uungwaji mkono wa Democrats ili kuweza kupata pesa za kujengwa ukuta huo.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Wale wanaompinga Trump waliokuwa wamekusanyika nje ya mkutano huo walikabiliana na polisi baada ya mkutano huo kumalizika

Katika hotuba yake bwana Trump alisema kuwa Democrats wanaliweka taifa la Amerika hatarini.

Alisema kuwa maafisa wa uhamiaji wanaofanya kazi eneo hilo wanasema kuwa ni muhimu kuzuia wahamiaji haramu kuingia Marekani.

Huku hotuba ya Trump ikishangiliwa ndani ya ukumbi, wale wanaompinga Trump waliokuwa wamekusanyika nje ya mkutano huo walikabiliana na polisi baada ya mkutano huo kumalizika.

Polisi walilazimika kutumia maji wa kuwasha wakati waandamanaji walianza kurusha mawe na chupa.

Mada zinazohusiana