Watu nchini Angola wamchagua rais mpya baada ya miaka 38

Supporters of Angola's Casa-CE party Haki miliki ya picha EPA
Image caption Vijana wanasema kuwa ajira ndiyo ajenda kuu

Watu nchini Angola wanapiga kura kumchagua rais mpya

Rais Jose Eduardo dos Santos amekuwa madarakani tangu mwaka 1979 na kuwa rais wa pili barani Afrika kuwa madarakani kwa kipindi kirefu zaidi.

Rais Santos hawanii tena uchaguzi huu, ambao waziri wa ulinzi Joao Lourenco anawania kama mgombea kupitia chama tawala cha MPLA.

Mpinzani wake mkuu anatarajiwa kuwa Isias Samakuva, kutoka chama cha hasimu wa MPLA, Unita.

Haki miliki ya picha .
Image caption Wagombea

Wachangazi wanasema kuwa chama cha MPLA ambacho kimekuwa madarakani tangua uhuru wa nchi hiyo mwaka 1975, kinaokana kuwa kitaibuka mshindi.

Chama cha tatu kwa ukubwa cha Casa-CE, kinaongozwa na Abel Chivukuvuku, ambaye alikuwa afisa wa cheo cha juu wa Unita wakati kilikuwa ni kundi la waasi.

Image caption Mwanamke huyu alipiga kura mapema leo

Baada ya vita, Angola ilikuwa moja ya nchi zilizokuwa aa uchumi uliikua kwa haraka zaidi duniani kutona na utajiri wake mkubwa wa mafuta.

Lakini wakati bei ya mafuta ilishuka miaka miwili iliyopita iliadhiri uchumi wote.

Ikiwa asimia kubwa ya watu wako chini ya umri wa maiak 35, watu hao ndio na watakuwa na uamuzi mkubwa.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Kampeni zimekuwa kubwa kabla ya kura

Mada zinazohusiana