Afrika Kusini yapiga mnada pembe za faru

Askari wa wanyama pori akipima pembe ya faru itakayotolewa katika shamba la bwana Hume
Image caption Askari wa wanyama pori akipima pembe ya faru itakayotolewa katika shamba la bwana Hume

Kwa mara ya kwanza Afrika Kusini inapiga mnada wa pembe za faru, moja kwa moja kupitia mtandaoni.

Soko hiyo imefanyika muda mfupi uliopita, ambapo mamia ya pembe zinazogharimu mamilioni ya dola kwa kilo, zinauzwa katika mnada huo.

Mara tu zitakaponunuliwa, mnunuzi hawezi kutoka na mzigo huo nje ya Afrika Kusini, kutokana na marufuku ya bidhaa za wanyama pori kote Duniani.

Mwaandalizi wa soko hilo la mnada John Hume, anamiliki vifaru elfu 15, kaskazini mwa mji mkuu Johannesburg.

Anasema kuwa anavuna pembe hizo bila ya ukatili kwa wanyama, kwa kufanya mnyama asihisi uchungu.

Mnada huo unafanyika licha ya kuwepo kwa upinzani kutoka kwa wana mazingira, ambao wanalalamika kuwa hatua hiyo itasababisha uwindaji haramu wa wanyama pori na kutatiza juhudi za kujaribu kuboresha idadi ya faru duniani, ambao huenda wakaangamia kabisa.