Boris Johnson aitembelea Libya kukabili uhamiaji haramu

Johnson akiwa na waziri mkuu wa Libya Fayez al-Sarraj (kulia)
Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza Boris Johnson amekuwa kiongozi wa juu wa kwanza kutoka nchi za Magharibi kutembelea mji wa Misrata uliopo Libya ndani ya miaka mitano.
Alifanya mazungumzo mafupi na viongozi wa ndani wa nchi hiyo katika sehemu ambayo maandamano dhidi ya kiongozi wa zamani wa taifa hilo Muammar Gaddafi yalianzia mwaka 2011.
Mapema alionana na waziri mkuu wa Libya anayeungwa mkono na umoja wa mataifa Fayez al-Sarraj.
Pauni milioni nne zitatumika kuondoa mabomu ya ardhini katika sehemu hii iliyokuwa inakaliwa na IS
Johnson ameitaja Libya kama mshirika mkuu wa Ulaya wa kukabiliana na uhamiaji haramu.
Amesema Uingereza itaisaidia Libya kuweka mpaka wa umeme utakaozuia wahamiaji hao Kusini mwa nchi hiyo.