Samsung wazindua toleo jipya la Galaxy Note 8

Image caption Kampuni hii inasema toleo hili litarusha heshima iliyopotea

Kampuni ya simu za mkononi ya Sumsung, imezindua simu yake mpya ya Galaxy Note 8, ambayo ni ya kisasa zaidi na yenye ushindaji zaidi katika soko.

Image caption Samsung inasema marekebisho yaliyofanyika ni makubwa

Hatua hii inakuja baada ya kampuni hii kupata msukosuko wa kibiashara ikiwa ni takribani mwaka mmoja tangu ilipotoa simu aina ya Galaxy note 7 ambayo betri zake zilikuwa zinalipuka hivyo kulazimika kutolewa sokoni.

Kampuni hii ya Sumsung kutoka Korea kusini, katika toleo hili jipya la simu ya Galaxy note 8 imekuja na vitu vipya katika teknolojia ya usalama, ambapo ina uwezo kutambua muonekano wa mmiliki wa simu, alama za vidole, mboni ya jicho na mfumo mpya wa kiusalama ujulikanao kama Samsung Bixby ambayo inatoa sauti maalumu za maelekezo ya kuweka ulinzi wa siri wa simu hiyo ubora mpya wa picha.

Image caption Note 8 inamfanya mtumiaji aweze kuzuia vitu asivyovitaka visionekane kwenye picha

Simu hii ya Note 8,imekuja na kioo chenye upana wa nchi 6.3 kutoka kona moja na nyingine,ongezeko la ukubwa wa nchi 0.1 ikilinganishwa toleo la S 8.