Kuwanyonyesha watoto: Simulizi kutoka kwa wanawake sita

Kuwanyonyesha watoto: Simulizi kutoka kwa wanawake sita

Agosti ni mwezi uliotengwa mahsusi kuangazia manufaa ambayo unyonyeshaji wa watoto huwa nayo kwa mama na mtoto.

Lakini siku hizi wanawake wengi wamekuwa wakisusia kuwanyonyesha watoto wao, au hata wanapowanyonyesha huwa si kwa muda uliopendekezwa.

Tunawaangazia wanawake sita ambao licha ya kukabiliwa na changamoto mbalimbali, wameamua kuwanyonyesha watoto wao.

Wamejitokeza kushiriki katika kampeni iliyoandaliwa na mwandishi wa zamani Kenya Janet Mbugua-Ndichu ya #IAMMotherhood.