Kwa Picha: Maua yachanuka jangwani Chile

Atacama Desert, Chile, 22 August 2017. Haki miliki ya picha EPA
Image caption Raia wa Chile pamoja na watalii kutoka nje ya nchi wamefika kujionea maua hayo

Maeneo ya jangwa la Atacama nchini Chile, ambalo ni miongoni mwa maeneo makavu zaidi duniani, yameota maua mengi baada ya mvua kunyesha bila kutarajiwa.

Tukio hilo la 'desierto florido' kwa maana ya 'maua jangwani' hutokea kawaida kila baada ya miaka mitano au saba mvua inaponyesha na kusababisha mbegu zilizozikwa kwenye mchanga kumea mimea ambayo huchanua maua.

Lakini maua ya sasa yametokea chini ya miaka miwili baada ya mengine kuchipuza mwaka 2015.

Zaidi ya aina 200 ya mimea inakua katika eneo hilo kwa sasa.

Tukio hilo la kutokea kwa maua jangwani huwavutia wageni na wataalamu wa mimea kutoka Chile na hata nje ya nchi hiyo.

Maafisa wa utalii nchini humo wamesema wanatumai maua hayo yataendelea kuchanua katika muda wa wiki kadha zijazo kwani mimea inayochanua maua humea katika nyakati tofauti.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Kwa mbali, maua hayo yanaonekana kama barafu
Haki miliki ya picha EPA
Image caption Maua hayo ni ya rangi mbalimbali, kuna ya rangi nyeupe...
Haki miliki ya picha EPA
Image caption ...ya rangi ya manjano...
Haki miliki ya picha EPA
Image caption ...na mengine ya rangi ya zambarau
Haki miliki ya picha EPA
Image caption Kawaida, eneo hilo ambalo hutumiwa kuandaa mashindano ya mbio za magari na pikipiki ya Atacama, huonekana hivi.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii