Wanandoa Waislamu walioachana walazimishwa kurudiana Chechnya

Wanawake wa Chechen wakiwa wamevalia mavazi ya kitamaduni Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Wanawake wa Chechen wakiwa wamevalia mavazi ya kitamaduni

Kiongozi wa kiimla wa Jamhuri ya Chenchen, Ramzan Kadyrov anaongoza kampeini ya kuwaunganisha wanawake na wanaume walioachana kwa kuwajumuisha viongozi wa dini ya kiislamu wanaowahubiria Uislamu.

Tume ilioteuliwa na bw Kadyrov inadai kuwaunganisha wapenzi 948 katika kipindi chawiki sita.

Pia meingiza Uislamu wa kihafidhina katika taifa hilo lililojitenga na Urusi

Lakini wanawake waliokuwa wameachwa kitambo wamelalamikia kwa kulazimishwa kurudiana na wapenzi wao. Mwanamke mmoja amesema kampeini hiyo ni ya ''kikatili.''

Kiongozi mmoja amesema mwanamume ana uwezo wa kuwa na wake wawili , iwapo itawanufaisha watoto.

Rasul Uspanov, katibu wa Chechen amesema '' kituo kikuu cha kutatua maswala ya uhusiano wa wanandoa na familia , amesema kuna kesi ambazo zimeripotiwa , baada ya kutalikiana , watoto wamekuwa wanaishi na baba yao, ambaye ameoa mke mwengine.

Baada ya kazi ya tume yetu, alimpata mkewe wa kwanza na hivi sasa anaishi na wake wote wawili kwa sababu kulingana na sheria ya kiislamu mwanamume anaweza kuwa na wanawake wanne, amesema.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Kiongozi wa kiimla nchini Chechen Ramzan Kadyrov

Wanaume ambao wako katika hali hiyo , wanaelewa kwamba ni vyema kwamba mama ya watoto anastahili kuishi na wanawe, kuliko kuwashughulikia ukiwa mbali huku wakipata mateso,alisema.

Lakini mwanamke mmoja kwa jina Bariyat, alinukuliwa na BBC ya Urusi, akisema ''Nimetalakiwa miaka 12 iliyopita na iwapo tume itanifuata basi mimi nitakataa.''

Ni hujuma miongoni mwa watu, alisema Bariyat anayeishi katika mji mkuu wa Grozny. ''Iwapo wapenzi wanawachana huwa ni wazi kwamba ulikuwa uamuzi wa mwisho.'' Amesema pia wakati mwengine huko Chechnya , wapenzi huoana bila kufahamiana lakini kwa kupendekezewa

Mkaazi wa Grozny kwa jina Zarema amenukuliwa akisema alilazimishwa kurudiana na mumewe kutokana na shinikizo ya Ramzan Kadyrov mwenyewe.

''Iwapo utakataa , inamaanisha unaenda kinyume na dini na tamaduni na pia mapenzi yake. Ni wazi ukilazimishwa kutoka pande zote mbili , ni lazima ukubali.''

Alipotangaza uzinduzi wa kampeini hiyo mwezi Julai, bw Kadyrov alisema watoto kutoka familia zilizotengana basi walikuwa katika hatari ya kuteuliwa na makundi ya kigaidi.

''Viongozi wa dini, wale wa vijiji na wilaya ,maafisa wakuu wa polisi ni sharti watafute chanzo cha wapenzi kutengana'',alisema.

Makundi ya kutetea haki za kibinadamu yamelaumu vikosi vya usalama vya bw Kadyrov kwa unyanyasaji mkubwa ikiwemo utekaji na kuwatesa wapinzani