Balozi wa Urusi nchini Sudan afariki katika kidimbwi cha kuogelea

Mirgayas Shirinsky Haki miliki ya picha EPA Ministry Russia
Image caption Mirgayas Shirinsky

Balozi wa Urusi nchini Sudan amepatikana amefariki katika kidimbwi cha kuogelea nyumbani kwake huko Khartoum.

Maafisa wa polisi wa Sudan wanasema kuwa uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa bwana Mirgayas Shirinsky alifariki kutokana na sababu za kimaumbile.

Ijapokuwa kifo chake hakijawekewa shauku yoyote, bwana Shirinsky ni mwanadiplomasia wanne kutoka Urusi kufariki katika afisi katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita.

Mnamo mwezi Februari, balozi wa Urusi katika Umoja wa Mataifa Vitaly Churkin alifariki kwa ghafla katika afisi yake mjini New York.

Mwezi mmoja kabla, balozi wa Urusi nchini Uturuki Andrei Karlov alipigwa risasi mjini Ankara na afisa wa polisi wa Uturuki aliyekuwa akipinga hatua ya Urusi kuingia nchini Syria