Venezuela yazifungia Televisheni mbili za Colombia

Mamlaka ya mawasiliano nchini humo imesema sababu zilizoainishwa ni muhimu
Image caption Mamlaka ya mawasiliano nchini humo imesema sababu zilizoainishwa ni muhimu

Venezuela imezifungia televisheni mbili kutoka nchini Colombia kurusha matangazo nchini humo.

Serikali ya Venezuela bado haijatoa sababu ya kufanya hivyo, lakini Rais Nicolas Maduro amewahi kuvituhumu baadhi ya vyombo vya habari vya Colombia kwa kuingilia mambo yake ya ndani.

Mmoja wa wamiliki wa televisheni hizo amesema anaamini zuio hilo limetokana na kuwasili nchini Colombia kwa Luisa Ortega ambaye amekuwa akimpinga Rais Maduro.

Image caption Luisa Ortega amekuwa akimlaumu Maduro kwa kuhusika na rushwa

Televisheni za Colombia zilizofungiwa ni RCN na Caracol.