Idd Seif akumbuka safari ya Dira ya Dunia TV

Idd Seif akumbuka safari ya Dira ya Dunia TV

Michezo imechukua nafasi kubwa sana katika matangazo ya Dira ya Dunia TV, tumewatuma waandishi wetu sehemu mbalimbali kutuletea habari moto moto za michezo kutoka zile za kimataifa na za nyumbani.

Idd Seif alikuwa mmoja wa waasisi wa meza ya michezo tangu Redio na baadae alijiunga na kikosi cha TV na kushughulika na Michezo na pia alikuwa mtayarishaji mkuu wa Sanaa.

Idd Seif ametutembelea na anakumbuka safari yetu katika miaka hiyo mitano.