Mvulana atumia funzo kutoka kwa filamu kumuokoa ndugu yake Marekani

Christa O'Connor with Dylan (left) and Jacob Haki miliki ya picha Patricia O'Blenes/C&G Newspapers
Image caption Christa O'Connor na wanawe huishi Roseville, karibu na Detroit

Nyota wa Hollywood Dwayne Johnson, almaarufu The Rock amemtaja mvulana wa miaka 10 kuwa "shujaa halisi" baada ya mvulana huyo kutumia mafunzo kutoka kwa filamu kumuokoa ndugu yake.

Jacob O'Connor kakake wa miaka miwili Dylan akielea kwenye kidimbwi cha kuogolea uso wake ukiwa kwenye maji.

Lakini badala ya kukimbia kuomba usaidizi alitumia mafunzo aliyoyapata kutoka kwa filamu aipendayo sana ya San Andreas.

Jacob, kutoka Roseville, Michigan, alifanikiwa kumtoa ndugu yake kutoka kwenye kidimbwi na kuanza kumpa huduma ya kwanza kumsaidia kuanza kupumua tena, kama alivyoona The Rock akifanya kwenye filamu hiyo.

Dylan baadaye alikimbizwa hospitalini na alipata nafuu kabisa.

Aliposikia kuhusu aliyoyafanya Jacob, Dwayne Johnson aliandika kwenye Twitter: "Kisa cha kuvutia sana....wewe ni shujaa halisi. Tunajivunia! DJ."

Mamake Jacob, Christa O'Connor aliambia BBC kwamba alifurahishwa sana na alichofanya Jacob.

"Nilishangaa kwamba alikumbuka alichokuwa ameona kwenye filamu hiyo, ambayo anaipenda sana na alikuwa ameitazama wiki iliyotanguliwa."

Haki miliki ya picha Patricia O'Blenes/ C&G Newspapers
Image caption Jacob (kushoto) alimuokoa kakake kwa kurudia aliyokuwa ameyaona The Rock akifanya kwenye filamu

Jacob aliambia vyombo vya habari: "Niliingiwa na wasiwasi nilipomuona Dylan kwenye kidimbwi...Nilikumbuka kwenye filamu ya San Andreas, baada ya tetemeko la ardhi, kisha kukatokea kimbunga na msichana alikuwa katika hatari ya kufa maji.

"Katika filamu nyingi, hilo ndilo jambo la kwanza watu hufanya (huduma ya kusaidia mtu kupumua). Jaribu kumuokoa mtu kwanza, na ikiwa hilo halisaidii, basi tafuta usaidizi."

Haki miliki ya picha Christa O'Connor
Image caption Jacob O'Connor na ndugu zake Gavin (kushoto) na Dylan (kati)

Dylan alikuwa amefungua milango miwili ya nyuma na kuingia kwenye bustani na alipokuwa akitembea akatumbukia kwenye kidimbwi cha kuogelea.

Mada zinazohusiana