Barcelona kumfanya Dembele kuwa mchezaji ghali

Ousmane Dembele wa Borrusia Dortmund Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Ousmane Dembele wa Borrusia Dortmund

Barcelona wanakaribia kumfanya mchezaji wa Borussia Dortmund Ousmane Dembele mchezaji wa pili aliye ghali zaidi katika historia.

Boruissia Dortmund ilikataa ombi la Barcelona kumunua mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20 anayeaminika kuwa na thamani ya Yuro milioni 100, mapema mwezi Agosti huku mchezaji huyo akipigwa marufuku kwa kukosa kufika mazoezini.

Kitita hicho hatahivyo kinakadiriwa kuwa chini ya Yuro milioni 222 ambazo PSG iliilipa Barcelona kumnunua Neymar mnamo mwezi Agosti.

Hathivyo kitita hicho kitakipiku kile kilichotolewa na Manchester United kumnunua Paul Pogba kutoka Juventus.

Mchezaji wa Ufaransa Dembele hajaichezea Dortmund tangu kombe la Supercup mnamo tarehe 5 Agosti.

Alijiunga na timu hiyo ya Bundesliga kutoka klabu ya Rennes kwa Yuro milioni 15 miezi 12 iliopita akiwa ameanza kucheza mwaka 2015.

Mada zinazohusiana