Wazungu waliomlazimisha mtu mweusi kuingia katika jeneza hatiani

Wakulima wazungu ,Theo Martins Jackson na mwenzake Willem Oosthuizen Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wakulima wazungu ,Theo Martins Jackson na mwenzake Willem Oosthuizen

Wakulima wawili wazungu nchini Afrika Kusini waliomlazimisha mtu mweusi kuingia katika jeneza wamepatikana na hatia ya jaribio la mauaji na utekaji nyara.

Victor Mlotshwa mwenye umri wa miaka 27 alipigwa na kulazimishwa kuingia katika jeneza na wawili hao Theo Martins Jackson na mwenzake Willem Oosthuizen mwaka 2016.

Wawili hao bado hawajahukumiwa. Walikuwa wamekana mashataka hayo.

Kesi hiyo ilizuia hisia kali nchini Afrika Kusini na kuangazia wasiwasi wa ubaguzi wa rangi miongoni mwa wakulima .

Bwana Mlotshwa aliripoti kisa hicho baada ya kanda ya video ya unyanyasaji huo kuonekana katika mtandao wa YouTube miezi kadhaa baadaye.

Katika hati ya kiapo ya mahakamani Jackson na Oosthuizen walisema hawakulenga kumuumiza bwana Mlotshwa lakini walitaka kumpatia funzo.

Image caption Victor Mlotshwa mwenye umri wa miaka 27 alipigwa na kulazimishwa kuingia katika jeneza

Huku Jaji Segopojte akitoa uamuzi wake katika mahakama ya Middelburg siku ya Ijumaa, wafuasi wa mwathiriwa huyo walisherehekea.

''Nafurahi kwamba hatimaye haki imepatikana'' , bwana Mlotshwa aliambia BBC.

Mada zinazohusiana