Watu 26 wafariki katika makabiliano na polisi India

Magari kadhaa yameteketezwa moto huko Panchkula Haki miliki ya picha AFP/GETTY IMAGES
Image caption Magari kadhaa yameteketezwa moto huko Panchkula

Yamkini watu 26 wameuwawa kaskazini mwa India, baada ya ghasia kutokea, mara baada ya mahakama moja nchini humo, kumhukumu Guru mmoja anyemiliki dhehebu lake na anayejiita mtu mzuri, kwa kosa la kuwabaka wanawake.

Idara ya polisi inasema kuwa baadhi ya waumini wa mtu huyo wanaodaiwa kufikia milioni moja, walianzisha ghasia ya kuwarushia polisi kila aina ya silaha ikiwemo mawe, mara tu mahakama ilipotoa hukumu hiyo.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Umati wa watu ukiharibu gari la Televisheni, baada ya mahakama kutoa hukumu hiyo huko Panchkula

Duru kutoka mji wa Panchkula zinathibitisha kuwa watu hao 26 kweli wamefariki, huku wawili wakiwa katika hali mahututi.

Image caption Gurmeet Ram Rahim Singh anasemekana kuwa na waumini wanaofikia milioni moja, India

Hii ni kwa mjibu wa taarifa kutoka makao makuu ya Polisi katika jimbo la Panchkula, kaskazini mwa India.

Awali kulikuwa na hofu ya kutokea fujo, baada ya kiongozi huyo wa kidini:- Gurmeet Ram Rahim Singh, alipopatikana na hatia ya kuwanyanyasa kingono waumini wake wawili wa kike, katika kesi hiyo ya mwaka 2002.

Haki miliki ya picha MANOJ DHAKA
Image caption Makumi kwa maelfu ya wafuasi wa Guru huyo wakimiminika mjini Chandigarh

Kisa hicho kinadaiwa kufanyika katika makao makuu ya kiongozi wa kundi hilo la Dera Sacha Sauda, iliyoko katika mji wa Sirsa, Kaskazini mwa India.

Image caption Ramani ya India