Mifuko ya plastiki kuwa marufuku Kenya

Jumapili tarehe 27 mwezi huu wa Agosti ndio siku ya mwisho kwa Wakenya kutumia mifuko ya kawaida ya plastiki.

Marufuku ya mifuko hiyo itaanza kutekelezwa Jumatatu. Baadhi wamebuni njia mbadala ya kubebea mizigo ikiwemo mifuko ya vitambaa, nyuzi au mikonge.