Trump aagiza watu waliobadili jinsia kutoajiriwa jeshini

Wanaharakati wa watu waliobadili jinsia wakianda,mana wakipinga agizo la rais Trump Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wanaharakati wa watu waliobadili jinsia wakiandamana wakipinga agizo la rais Trump

Rais Donald Trump ameagiza idara ya ulinzi Marekani kusitisha uajiri katika jeshi wa watu waliobadilisha jinsia zao.

Trump aliashiria hatua hiyo ghafla katika ujumbe kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter mwezi jana.

Katika ilani kwa waziri wa ulinzi Jim Mattis, Trump amesema Pentagon ni lazima irudishe marufuku hiyo.

Idara hiyo ya ulinzi itaamua hatma ya watu ambao wamebadiisha jinsia na ambao tayari wanalitumikia jeshi .

Agizo hilo pia linasitisha nafasi ya wanajeshi wa kiume na wa kike kufanyiwa upasuaji wa kubadili jinsia zao.