Biashara za Korea Kaskazini zapigwa marufuku China

Waziri wa maswala ya kigeni nchini China Wang Yi
Image caption Waziri wa maswala ya kigeni nchini China Wang Yi

China imepiga marufuku watu na makampuni ya Korea kaskazini kufanya biashara China.

Tangazo la marufuku hiyo lililotolewa na wizara ya biashara Beijing, linaambatana na vikwazo vya umoja wa mataifa vilivyoidhinishwa mapema mwezi huu kufuatia mradi wa Pyongyang kufanyia majiribio makombora yake.

Wizara hiyo pia imeeleza kuwa maombi ya uwekezaji kutoka kwa Korea kaskazini yatakatiliwa.