Jeshi la Iraq lakabiliana vikali na IS mjini Tal Afar

Majeshi ya Iraqi inasema kuwa, inakaribia kuudhibiti mji wa Tal Afar kwa kuwaangamiza wanamgambo wa IS Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Majeshi ya Iraqi inasema kuwa, inakaribia kuudhibiti mji wa Tal Afar kwa kuwaangamiza wanamgambo wa IS

Wanajeshi wa Iraqi wamefurahia ushindi wao wa kutwaa maeneo ya katikati mwa Wilaya ya mji wa Tal Afar, wakati ambapo nguvu ya wanamgambo Islamic State, ikisambaratika.

Baada ya wiki moja ya mapigano makali, jenerali mkuu anayeongoza oparesheni hiyo, anasema kuwa, kwa mara nyingine tena bendera ya taifa la Iraq inapepea katika eneo la Citadel.

Lakini Jenerali Abdulamir Yarallah, anakiri kuwa mapigano makali sasa yanashuhudiwa viungani mwa maeneo ya kaskazini mwa mji huo.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Siku ya Ijumaa maeneo muhimu ya Islamic State mjini Tal Afar yalishambuliwa na ndege za kivita za jeshi la Iraq

Mwaandishi wa BBC, anasema kuwa, serikali ya Iraq, inatarajia kutangaza ushindi wake wa mwisho wa kuutwa mji huo, katika kipindi cha siku kadhaa zijazo.

Mji Tal Afar unatajwa kama ngome ya mwisho ya I-S nchini Iraq, lakini wanajihadi hao wangali wakidhibiti maeneo yote mawili ya mpakani, kati ya Iraq na Syria, na maeneo ya Hawija -- mji ulioko kati ya Mosul na mji mkuu wa Iraqi, Baghdad.

Image caption Ramani ya Iraq