Ali Kiba, Nandy, Bebe Cool na Nyashinski kuwania tuzo za AFRIMA

Msanii wa Tanzania Ali Kiba kuwania tuzo za AFRIMA
Image caption Msanii wa Tanzania Ali Kiba kuwania tuzo za AFRIMA

Wanamuziki wa Tanzania, Uganda na Kenya akiwemo Ali Kiba, Nandy, Bebe Cool na Nyanshiski ni miongoni mwa nyota 18 wa muziki walioteuliwa kuwania tuzo za All Africa Music Awards {AFRIMA} zinazotarajiwa kuandaliwa mnamo mwezi Novemba.

Wengine walioteuliwa ni pamoja Bebe Cool wa Uganda , Yemi Alade, AKA,

Runtown, Nasty C, Eddy Kenzo, Locko, Anselmo Ralph, Jah Prayzah, Busiswa, Amanda Black,

Kiff No Beat, Mafikizolo, Micasa na Olamide.

Orodha ya walioteuliwa ilitangazwa mwezi Agosti katika hoteli ya Renaissance mjini Lagos, Nigeria.

Orodha ya walioteuliwa ina makundi 33, ikiwemo 10 ya kieneo mbali na mengine 23 huku nyota wa Coke studio wakijizolea nafasi 25.

Katika tuzo nyengine ya Afrima ya baadaye nyota wengine wa Coke studio wameteuliwa katika kundi la kibara.

Wao ni Kiff No Beat (Ivory Coast) Mafikizolo na Mi Casa kutoka Afrika Kusini katika kundi bora la muziki Afrika.

Kwa kundi bora zaidi barani Afrika walioteuliwa ni Anselmo Ralph (Angola) na Alikiba (Tanzania).

Wimbo wa Aje ulioimbwa na Alikiba akishirikiana na MI pia umeteuliwa katika kundi la muziki bora uliofanywa kwa ushirikiano pamoja na Jah Prayzah's Watora Mari akishirikiana na Diamond na Supporter

ilioimbwa na Locko akishirikiana na Mr Leo.