Gurmeet Ram akutwa na hatia ya ubakaji

India
Image caption Gurmeet Ram Rahim Singh mtuhumiwa

Maafisa usalama kaskazini mwa India jimboni Haryana na Punjab wamekuwa katika tahadhari ya hali ya juu kabla ya hukumu tata dhidi ya mhubiri mkuu wa dini nchini humo kukutwa na hatia ya ubakaji.

Wafuasi wa Gurmeet Ram Rahim Singh walianzisha vurugu kufuatia hukumu dhidi ya kiongozi huyo ilipotishwa mwishoni mwa wiki. Inaarifiwa kuwa watu thelathini na nane wamefariki dunia katika ghasia hizo.

Kufuati hali hiyo Shule na vyuo waliamriwa kufungwa katika mji wa Rohtak, mahali ambapo mahakama maalum iliandaliwa ndani ya jela moja.

Wakaazi wa eneo hilo wameshauriwa kutotoka majumbani kwao . Mtuhumiwa alijiweka katika hali ya utakatifu maishani mwake , ambaye anadai kuwa na mamilioni ya wafuasi, anakabiliwa na kifungo cha chini cha miaka saba jela na kifungo cha maisha jela.

Serikali ya BJP katika jimbo hilo imekumbwa na upinzani mkubwa na lawama ya kushindwa kudhibiti vurugu hizo.